Main Slider

‘Wabunge leteni mapendekezo mjengewe mahakama



SERIKALI imesema ina fedha za kujenga mahakama na kutoa changamoto kwa wabunge kutumia fursa kwa kupeleka hoja na mapendekezo ya msingi ili waweze kujengewa mahakama hizo.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe alisema zimetengwa fedha kwa ajili ya kujenga mahakama kiasi cha Sh bil 34.3 na kwamba fedha hizo zitatumika kujenga mahakama za mwanzo 50, mahakama za wilaya 20 na Mahakama Kuu mpya katika mikoa ya Mara na Kigoma.
Alikuwa akimjibu Mbunge wa Mbagala, Issa Mangungu (CCM), ambaye kwenye swali lake la nyongeza alimwambia Waziri kuwa Mbagala vipo viwanja viwili ambavyo serikali inaweza kujenga mahakama za mwanzo.
Waziri Mwakyembe alimshukuru mbunge huyo kwa kutoa viwanja na kumtaka kuweka rekodi kwa maandishi na kuvikabidhi vikiwa na nyaraka halali na kuwataka wabunge wengine kupeleka maombi yenye hoja zinazoeleweka ili wajengewe mahakama hizo.
Katika swali lake la msingi, Mangungu alisema jimbo hilo lina wakazi 800,000 lakini serikali imeshindwa kujenga mahakama katika jimbo hilo kwa kuzingatia idadi kubwa ya wakazi.
Waziri Mwakyembe akijibu hoja hiyo alimhimiza Mbunge na uongozi wa mkoa wa Dar es Salaam na wilaya zake kutoa viwanja vyenye nyaraka rasmi ili uwekwe mpango wa dharura wa ujenzi wa mahakama za mwanzo kwenye maeneo yenye uhitaji.
Alisema mkoa wa Dar es Salaam kwa sasa una wilaya tano kiutawala na kata zaidi 102 zenye idadi ya wakazi zaidi ya milioni tano wanaohitaji huduma hiyo muhimu na kukiri kuwa mkoa huo unahitaji mahakama za kisasa katika wilaya tano na mahakama za mwanzo 102 angalau kukidhi kila kata ukilinganisha na mahakama zilizop

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni