Main Slider

Wapatiwa bilioni 470/- kuboresha mfumo



WANANCHI wa Mkoa wa Arusha wataachana na shida ya kupata maji safi katika kipindi cha miaka miwili na nusu, baada ya Serikali kupitia Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kuipatia Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWSA), Sh bilioni 476 za kuboresha mfumo wa maji safi.
Akizungumza jana hapa katika mkutano wa wadau wa mapitio ya mkataba wa huduma kwa wateja wa mamlaka hiyo, Mkurugenzi wa AUWSA, Ruth Koya aliwatoa wasiwasi wananchi wa mkoa huo kuwa hawatakuwa na mgawo wa maji katika muda mfupi baada ya kupatikana kwa asilimia 100.
Koya alisema licha ya upatikanaji maji safi kwa uhakika, pia itasambaza mabomba makubwa ya kisasa ya kupitishia maji taka, ambayo kwa sasa ni kero kwa wateja kutokana na mabomba yaliyopo kuchakaa na sehemu kubwa ya wananchi kukosa huduma hiyo.
Alisema tayari wameshapokea fedha za awali kwa ajili ya kuanza mradi huo, ndani ya miaka mitatu ambapo wameshampata mkandarasi na yupo kazini katika kutafuta vyanzo vya maji vikubwa. Mradi huo unapanga kununua jenereta kubwa ya Sh milioni 76 ili kuwa na umeme wa uhakika wakati wote na kutoa huduma bila kusitisha.
Mwenyekiti mpya wa Bodi ya AUWSA, Dk Job Laizer, aliwaomba wananchi kutoa maoni yao ya kuboresha mkataba huo wa 2013/2016 ili uendane na hali halisi ya sasa na uwe endelevu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni