Mwenyekiti wa Z4news ametoa nafursa kwa
vijana wanao imba muziki wa bongo flever kujiunga kwenye kundi lake la
muziki ili kuboresha zaidi wasani wachanga katika tasinia hiyo
hata hivyo mwenye kiti alisema kua
anatoa nafasi hiyo kwa vijana wawili bila ya kujali jinsia vijana
watakao fanya muziki kama maisha yao pia wanamuziki hao wawe na ubunifu
tofauti na wasani waliopo kwenye tasnia ''amesema
ninawataka vijana wawili wenye uwezo
wakuimba kila aina ya muziki na wanoa jua nini maana ya maisha mimi nina
hajiri moja kwa moja nimetoa fursa hii kwa ajili ya kuleta mabadiliko
mwaka ujao tukijaliwa uzima kwahiyo vijana naomba mjitokeze hili
kuonyesha uwezo wenu ''amesema
aliendelaea kusisitiza kua yupo tayari
muda wowote watakapo patikana wasanii hao atawapeleka studio na
kuwatabulisha kwenye tasnia ya muziki..
Kwa mawasiliano zaidi piga 0658894174
www.Mgazija blog
Main Slider
SPIKA WA BUNGE ATETA NA MKUU WA CHAMA CCM
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana alipomtembelea katika Ofisi Ndogo za CCM zilizopo Mtaa wa Lumumba Jijini Dar es Salaam.

Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akiwasili katika Ofisi Ndogo za CCM zilizopo Mtaa wa Lumumba Jijini Dar es Salaam alipofika kuzungumza na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana .
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akongozana na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Abdulrahman Kinana baada ya kuwasili alipomtembelea na kuzungumza naye katika Ofisi Ndogo za CCM zilizopo Mtaa wa Lumumba Jijini Dar es Salaam.

Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akimsikiliza Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Abdulrahman Kinana alipomtembelea na kuzungumza naye katika Ofisi Ndogo za CCM zilizopo Mtaa wa Lumumba Jijini Dar es Salaam.

Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (katika) akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana (kushoto) na Msemaji wa CCM Christopher Ole Sendeka (kulia) wakati alipomtembelea Katibu Mkuu wa CCM.Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akiagana na Msemaji wa CCM Christopher Ole Sendeka mara baada ya kuzungumza na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana katika Ofisi Ndogo za CCM zilizopo Mtaa wa Lumumba Jijini Dar es Salaam.
MVUA ZA VULI KUNYESHA CHINI YA WASTANI TMA
mamlaka ya hewa tanzania (TMA) imetangaza kuanza kwa msimu wa mvua katika miezi ya octoba, novemba na desemba huku ikisema mvua hizo zinatarajiwa
za chini ya wastani zitaathiri kilimo cha uzalishaji mazao kutokana na uchache wake pia alisema kutokana na uchache huo pia huathiri upatikanaji wa maji
safi na salama. Dk. kijazi amesema kwa miezi hiyo mvua chache zinatarajiwa katika maeneo mengi wakati maeneo ya pembezoni mwa ziwa victoria pamoja
na yale ya kusini mwa nchi mvua zinatarajiwa kuwa kuridhisha. Alifafanua kuwa katika maeneo mengi ya nchi, mvua hizo zinatarajiwa kuchelewa kuanza
maeneo ya ukanda wa ziwa victoria na maeneo machache ya pwani ya kaskazini. Dk, kijazi alisema vipindi vingi vikavu vinatarajiwa kusababisha unyevunyevu
mdogo katika udongo na hiyo kuathiri ustawi wa mazao ya kilimo katika maeneo mengi ya nchi.
Miriam Msuya na mwenzake wasomewa upya mashitaka ya mauaji
ALIYEKUWA mke wa bilionea maarufu jijini Arusha, marehemu Erasto Msuya, Miriam Msuya na mwenzake, wamesomewa upya mashitaka ya kumuua, dada wa bilionea huyo, Aneth Msuya.
Miriam na mfanyabiashara Revocatus Muyela (40), walisomewa upya mashitaka yao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es salaam, baada ya upande wa Jamhuri kuwafutia mashitaka, kisha wakawekwa chini ya ulinzi wa askari na baada ya muda walisomewa upya mashitaka yao mbele ya Hakimu Mkazi, Magreth Bankika.
Wakili wa Serikali Diana Lukondo amedai, Mei 25 mwaka huu katika eneo la Kibada, Kigamboni, Dar es salaam, washitakiwa walimuua Aneth.
Soma Habarileo Septemba 7 kwa habari zaidi
Bei ya tumbaku duniani yadoarora
ZAO la tumbaku limekuwa linapigwa vita duniani na kusababisha bei yake kudorora, imeelezwa.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William ole Nasha alikiri kuwa zao hilo limekuwa likikabiliwa na changamoto kubwa duniani na kusababisha bei kudorora na soko lake kupungua.
“Nakiri zao hili ni zao linalokabiliwa na upinzani mkubwa sana duniani... ni zao ambalo naweza kusema ‘limeshetanishwa’ na matokeo yake bei yake imedorora sana, wanunuzi wenyewe hakuna,” alisema.
Nasha alikiri kudorora kwa bei ya tumbaku ni shida ya duniani kote. Hata hivyo, serikali inatafuta fursa ya masoko kwa ajili ya zao la tumbaku hapa nchini.
Alieleza hayo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Serengeti, Ryoba Marwa (CCM) aliyehoji tumbaku haina soko na serikali itajenga lini kiwanda cha kuchakata tumbaku.
Katika swali la msingi, Marwa alitaka kufahamu serikali inakabiliana vipi na changamoto ya zao la tumbaku kukosa masoko, ikiwemo tumbaku ya wilaya ya Serengeti na itasaidiaje upatikanaji wa kampuni zaidi ya moja kununua tumbaku ndani ya wilaya hiyo.
Akijibu swali hilo, Nasha alisema zao la tumbaku linapigwa vita na kwamba hapa nchini wanunuzi ni wanne na kukiri kuwa hata katika nchi zingine hawana mnunuzi wa tumbaku zaidi ya wanne.
Hata hivyo, Naibu Waziri huyo alisema serikali inatafuta fursa ya masoko na kwamba hivi sasa inaangalia soko la China na fursa ya soko la shisha Misri.
Wapatiwa bilioni 470/- kuboresha mfumo
WANANCHI wa Mkoa wa Arusha wataachana na shida ya kupata maji safi katika kipindi cha miaka miwili na nusu, baada ya Serikali kupitia Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kuipatia Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWSA), Sh bilioni 476 za kuboresha mfumo wa maji safi.
Akizungumza jana hapa katika mkutano wa wadau wa mapitio ya mkataba wa huduma kwa wateja wa mamlaka hiyo, Mkurugenzi wa AUWSA, Ruth Koya aliwatoa wasiwasi wananchi wa mkoa huo kuwa hawatakuwa na mgawo wa maji katika muda mfupi baada ya kupatikana kwa asilimia 100.
Koya alisema licha ya upatikanaji maji safi kwa uhakika, pia itasambaza mabomba makubwa ya kisasa ya kupitishia maji taka, ambayo kwa sasa ni kero kwa wateja kutokana na mabomba yaliyopo kuchakaa na sehemu kubwa ya wananchi kukosa huduma hiyo.
Alisema tayari wameshapokea fedha za awali kwa ajili ya kuanza mradi huo, ndani ya miaka mitatu ambapo wameshampata mkandarasi na yupo kazini katika kutafuta vyanzo vya maji vikubwa. Mradi huo unapanga kununua jenereta kubwa ya Sh milioni 76 ili kuwa na umeme wa uhakika wakati wote na kutoa huduma bila kusitisha.
Mwenyekiti mpya wa Bodi ya AUWSA, Dk Job Laizer, aliwaomba wananchi kutoa maoni yao ya kuboresha mkataba huo wa 2013/2016 ili uendane na hali halisi ya sasa na uwe endelevu
‘Wabunge leteni mapendekezo mjengewe mahakama
SERIKALI imesema ina fedha za kujenga mahakama na kutoa changamoto kwa wabunge kutumia fursa kwa kupeleka hoja na mapendekezo ya msingi ili waweze kujengewa mahakama hizo.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe alisema zimetengwa fedha kwa ajili ya kujenga mahakama kiasi cha Sh bil 34.3 na kwamba fedha hizo zitatumika kujenga mahakama za mwanzo 50, mahakama za wilaya 20 na Mahakama Kuu mpya katika mikoa ya Mara na Kigoma.
Alikuwa akimjibu Mbunge wa Mbagala, Issa Mangungu (CCM), ambaye kwenye swali lake la nyongeza alimwambia Waziri kuwa Mbagala vipo viwanja viwili ambavyo serikali inaweza kujenga mahakama za mwanzo.
Waziri Mwakyembe alimshukuru mbunge huyo kwa kutoa viwanja na kumtaka kuweka rekodi kwa maandishi na kuvikabidhi vikiwa na nyaraka halali na kuwataka wabunge wengine kupeleka maombi yenye hoja zinazoeleweka ili wajengewe mahakama hizo.
Katika swali lake la msingi, Mangungu alisema jimbo hilo lina wakazi 800,000 lakini serikali imeshindwa kujenga mahakama katika jimbo hilo kwa kuzingatia idadi kubwa ya wakazi.
Waziri Mwakyembe akijibu hoja hiyo alimhimiza Mbunge na uongozi wa mkoa wa Dar es Salaam na wilaya zake kutoa viwanja vyenye nyaraka rasmi ili uwekwe mpango wa dharura wa ujenzi wa mahakama za mwanzo kwenye maeneo yenye uhitaji.
Alisema mkoa wa Dar es Salaam kwa sasa una wilaya tano kiutawala na kata zaidi 102 zenye idadi ya wakazi zaidi ya milioni tano wanaohitaji huduma hiyo muhimu na kukiri kuwa mkoa huo unahitaji mahakama za kisasa katika wilaya tano na mahakama za mwanzo 102 angalau kukidhi kila kata ukilinganisha na mahakama zilizop
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)

